PEDRO ASISITIZA "MIMI NI WA HAPAHAPA STANFORD BRIDGE"

STRAIKA wa matajiri wa Stanford Bridge, Pedro amesisitiza azma yake ya kuendelea kubaki Chelsea licha ya kuweko na taarifa kuwa anajipanga kwa ajili ya kurejea Hispania.

Pedro alijiunga na “The Blues” akitokea Barcelona kwa dau la pauni mil 21.4 lakini taarifa za hivi sasa zinasema hana mpango wa kuondoka katika Ligi ya premier.

Klabu ya Atletico Madrid imekuwa ikitajwa katika orodha ya timu zinazomwania straika huyo mwenye umri wa miaka 28.
Hatua ya Pedro kuweka bayana azma ya kutotaka kuondoka “Darajani” inatokana na ukweli kwamba ameanza kuaminiwa na kocha wa sasa, Antonio Conte.

“Nina furaha nikiwa hapa. Nayazungumza haya kwa imani ya moyoni. Ninajivunia kuwa katika klabu kubwa.”

“Nina furaha na mashabiki wa timu hii. Ingawa ni ukweli kuwa hali ya mambo si shwari hata kidogo lakini kwa pamoja tunaweza tukaipandisha timu kutoka hapa.”

“Ninaamini kwa kocha Antonio Conte. Ni kati ya makocha wazuri na klabu ina matarajio makubwa kwake. Najisikia vizuri.”


“Tayari ameonyesha imani kubwa kwangu nami nina imani kubwa kwake. Ninaamini chini ya Conte timu imeonyesha dhamira ya kupambana kwa ajili ya ubingwa wa premier msimu huu,” alisisitiza Pedro.

No comments