PHILLIPE COUTINHO AZIKUBALI FALSAFA ZA JURGEN KLOPP

KIUNGO wa Liverpool, Phillipe Coutinho amezikubali fomesheni na mbinu za kocha wa timu hiyo, Jurgen Klopp.

Coutinho amerudi uwanjani baada ya kuwa majeruhi kwa muda mrefu na juzi alikuwa anatazamiwa kucheza mechi ya marudio ya Kombe la FA dhidi ya Plymouth.

“Klopp ni kocha mzuri kwani amefanya kazi kubwa ya kuimarisha beki ya timu yetu,” alisema Coutinho.


Coutinho alieleza kufanya vizuri kwa kikosi hicho msimu huu ni matunda ya kazi ya Klopp.

No comments