Habari

PICHA 12: MASHAUZI CLASSIC WALIVYOKINUKISHA MKESHA WA MWAKA MPYA MANGO GARDEN

on

Moja ya viwanja vilivyolamba show za uhakika siku ya mkesha wa Mwaka
Mpya, ni Mango Garden Kinondoni.
Wajanja wote wa Kinondoni walikusanyika hapo na kuwashuhudia Mashauzi
Classic wakikinukisha kwa bonge la show.
Lile songi jipya la Isha Mashauzi “Radhi ya Mama” likazidi kuwa tishio
kwa namna lilivyowapagawisha mashabiki waliofurika Mango Garden.
Lakini jana pia kulikuwa na zawadi nyingine kutoka Mashauzi Classic,
wimbo mpya wa Saida Mashauzi “Usiforce Tufanane” nao ulitambulishwa na kuwakuna
watu vilivyo.

Shuhudia picha 12 za onyesho hilo la mkesha wa Mwaka Mpya kutoka kwa
Mashauzi Classic.
Isha Mashauzi akiimba wimbo wake mpya “Radhi ya Mama”
 Hashim Said jukwaani
 Isha Mashauzi akipagawisha
 Isha Mashauzi akikusanya kijiji
 Mwimbaji wa zamani wa Mashauzi Naima Mohamed akifanya mzaha na Kali Kitimoto jukwaani
 Abdumalick na msanii wa filamu za kibongo Baba James
 Mariam Kasola akitesa na moja ya nyimbo za Mashauzi Classic
 Mkude akicharaza solo gitaa
 Saida Mashauzi akikuambia “Usiforce Tufanane”
 Shangwe zilizokuwepo Mango Garden jana usiku
 Shebby wa Kumwaga na bass lake
Isha Mashauzi ndani ya Mango Garden jana usiku

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *