PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG AMWAGA CHOZI GABON KUTOLEWA MATAIFA YA AFRIKA

NAHODHA wa timu ya taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang amemwaga chozi baada ya kutolewa katika hatua ya makundi ya michuano ya mwaka huu ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCOM).

Gabon ambayo ni mwenyeji wa fainali hizo imeambulia nafasi ya tatu katika Kundi A na hivyo kushindwa kusonga mbele badala yake nafasi hiyo kuwaendea Burkina Faso na Cameroon.

Akizungumza kwa masikitiko Aubameyang alisema ameumia sana kuona wameshindwa kuifunga Cameroon katika mechi ya mwisho ya Kundi A kwa kutoka sare ya 0-0.

“Ni huzuni kwetu sote lakini binafsi nimesikitika sana, nilikosa bao la wazi katika dakika ya tatu ya mchezo, pengine ningefunga tungeweza kuwamaliza kabisa Cameroon na ushindi wowote ungutupeleka robo fainali,” alisema.


Kocha wa Gabon, Jose Antonio Camacho aliyeichukua timu hiyo siku 43 kabla ya kuanza kwa mashindano hayo kuchukua nafasi ya Jorge Costa, ni miongoni na waliokunwa na kiwango katika kipindi cha miaka 23 iliyopita.

No comments