POLISI WAMNASA ALIYECHORA DILI LA KUIBIWA KWA KIM KARDASHIAN

KIKOSI cha polisi mjini Paris, Ufaransa kimesema kuwa kimewatia mbaroni watu 17 akiwemo mshukiwa mkuu aliyechora dili la kuibiwa kwa mwigizaji Kim Kardashian.

Polisi wamesema kuwa mshukiwa mkuu wa tukio hilo lililotokea Oktoba, mwaka jana amenaswa baada ya kufuatilia kwa umakini pichwa zilizonaswa na kamera zilizotegeshwa.

Katika tukio hilo, Kim Kardashian ambaye ni mke wa Kanye West aliporwa vito vya thamani ikiwemo pete ya ndoa ya dhahabu yenye thamani ya dola za Kimarekani mil 4.


Tayari watu wane wameshahukumiwa kifungo kuhusiana na tukio hilo la wizi lililotokea kwenye hoteli moja.

No comments