KLABU ya Porto ya nchini Ureno inajiandaa kutuma ofa ya pauni mil 23 wakitaka saini ya straika wa Sevilla FC, Samir Nasri.

Taarifa za ndani ya klabu ya Porto zinasema kuwa Nasri amewekwa katika orodha ya wanandinga wanaowaniwa na vinara hao wa Ureno .

Awali, Porto walimweka katika orodha ya usajili wa majira ya kiangazi mwaka jana, lakini taarifa za asa zinasema kuwa wanambakiza straika huyo katika usajili wa kiangazi.

Lakini hatua ya wareno hao inaweza kudunda kwa sababu klabu hiyo ya Sevilla imekana kila hatua ya kuondoka kwa mchezaji yeyote katika kikosi chao.

Wakinukuliwa, Porto wamesema kuwa klabu yao haina mpango wa kuuza mchezaji katika kipindi cha uhamisho cha majira ya kiangazi.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac