POSHO YAVURUGA MAANDALIZI YA ZIMBABWE KUSHIRIKI MASHINDANO YA AFRIKA

SUALA la posho limetibua maandalizi ya Zimbabwe la kushiriki kwenye mashindano ya Afrika.

Mastaa wa Zimbabwe waligoma kupanda ndege Jumamosi iliyopita kwa ajili ya kwenda Cameroon kucheza mechi ya kirafiki.

Nyota hao wanataka kupewa posho ya dola za Marekani 5,000 (sh. mil 10.7), baada ya kukata tiketi ya kushiriki katika mashindano hayo wakigomea dola 1,000 (sh. mil 2.1) walizopangiwa na ZIFA.

Walikwenda mbali zaidi na kukataa kula chakula cha jioni na makamu wa rais wa Zimbabwe, Emmerson Munangagwa kwa ajili ya kuwaaga.


Msemaji wa ZIFA, Xolisani Gwesela alikaririwa akisema kuwa mzozo huo umemalizika na kila kitu kilikuwa shwari.

No comments