RAIS MSTAAFU WA VALENCIA AMPONDA GARY NEVILLE... asema ndie kocha bomu zaidi kuwahi kuinoa timu hiyo

RAIS wa zamani wa Valencia, Paco Roig amemponda Gary Neville kuwa ndie kocha bomu zaidi kuwahi kuinoa timu hiyo.

Neville alitimuliwa kuifundisha timu hiyo mwaka jana baada ya kukaa nayo kwa miezi mine.

Mmiliki wa timu hiyo, Peter Lim alimuingiza Neville akiamini angeleta mafanikio katika kikosi hicho.

Neville akaisimamia timu hiyo mechi 28 na kujikuta ikifungwa michezo yote.


“Nina mashaka na uelewa wa mmiliki wa timu kuhusu soka maana alimleta Neville baada ya kuona anafanya uchambuzi katika televisheni na matokeo yake wote tuliyaona, aliondoka na rekodi mbovu zaidi kuliko makocha wote waliopita hapa,” alisema Roig.

No comments