RAPA FAIZ ATANGAZA UJIO WA VIDEO YA WIMBO WAKE UITWAO "WEHDONE SIR"

RAPA Falz ametangaza rasmi ujio wa video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la “Wehdone Sir.”

Falz amesema video ya wimbo huo uliotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu utakuwa moja ya kazi bora za mwaka 2017 na akawataka mashabiki wake kuipokea kwa mikono miwili.

“Napenda kuwaambia mashabiki wangu kuwa naachia video ya wimbo wangu uitwao “Wehdone Sir”,” alisema Falz.


Mshindi huyo wa tuzo ya msanii bora wa mwaka 2016 alisema kuwa “Wehdone Sir” imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu.

No comments