Habari

RASHFORD: MSIFIENI MOURINHO, MSINISIFIE MIE

on

MSHAMBULIAJI kinda wa Manchester United Marcus Rashford amesema sifa zimwendee kocha Jose Mourinho kwa yote aliyofanya dimbani katika mchezo dhidi ya West Ham.
Rashford aliingizwa dakika ya 58 na kutengeneza bao la kwanza lililofungwa na Juan Mata dakika tano baadae na kuisababishia Manchester United kuibuka na ushindi wa 2-0 London Stadium.
Akizungumza baada ya mchezo, Rashford mwenye umri wa miaka 19 akasema maelekezo ya kocha ndiyo yaliyomwezesha kupika bao la kwanza.
Alipoulizwa ni ujumbe gani alipewa na Mourinho wakati akiingia uwanjani, Rashford alisema: “Aliniambia nibakie pembeni ili kumsumbua ‘fullbeki’ na ikazaa matunda. Hakika nilikuwa nafuata malekezo ya kocha.
“Nina furahia kuvuna pinti tatu, sasa tunaanza kunusa ‘top four’. Kuna mbanano mkubwa kati ya nafasi ya sita hadi ya pili hivyo tunapaswa kufanya vizuri kila mechi inayokuja mbele yetu”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *