REAL MADRID, BARCELONA WAKUTANA KATIKA VITA YA KUMWANIA VICTOR LINDELOF

KLABU mahasimu katika La Liga; Real Madrid na Barcelona zimeingia katika vita ya usajili wa msimu ujao na kujikuta wakimwania kwa pamoja Victor Lindelof.

Pamoja na vigogo hao wa jiji la Hispania, pia Manchester United wanatajwa katika mbio hizo za kumwania nyota huyo wa klabu ya Benfica.

Mlinzi huyo kijana amekuwa katika kwango bora katika msimu huu kiasi cha kuzigombanisha timu mbalimbali lakini Sky Sporty imezitaja Barca na Real kuwa ndizo zilizoonyesha nguvu kubwa ya kupata saini yake.

Imebainika kuwa Benfika imesitisha nia ya kumweka sokoni beki huyo baada ya kuondoka kwa beki wao mahiri, Renato Sanches.

No comments