REAL MADRID KUWEKA REKODI YA LA LIGA KWENYE MECHI YAO DHIDI YA SEVILLA LEO?

REAL Madrid inawania kuweka rekodi ya La Liga wakati itakapowakabili Sevilla katika mechi itakayopigwa leo.

Miamba hiyo ya soka imefunga kwenye mechi 28 mfululizo za Ligi hiyo.

Real Madrid ikipata bao leo ina maana kuwa itafikia rekodi iliyoiweka msimu wa 2013/14 wakati ikiwa chini ya Carlo Ancelotti ya kufunga mechi 29 mfululizo.


Mara ya mwisho kwa timu hiyo kutopata bao katika mechi ya La Liga ilikuwa Februari 27, 2016 wakati ilipofungwa bao 1-0 na Atletico Madrid.

No comments