REAL MADRID YAJITOSA VITA YA KUWANIA SAINI YA RAHEEM STERLING

KATIKA orodha ya usajili wa Real Madrid, kuna jina la Raheem Sterling na wameapa kula sahani moja na timu zinazohitaji saini ya straika huyo wa Manchester City.

Taarifa kutoka Madrid zinasema kuwa Sterling ametajwa katika orodha ya majina ya usajili wa majira ya joto mwaka huu.

Hata hivyo, straika huyo wa kimataifa wa England amenukuliwa akiweka bayana nia yake ya kutaka kuendelea kukipiga katika kikosi cha timu yake ya sasa ya Manchester City.

Akinukuliwa Sterling alisema kwa sasa hana sababu ya kuzungumzia wetesi za usajili ilihali yuko ndani ya mkataba katika kikosi cha matajiri hao wa jiji la Manchester.      

“Huwezi kuzungumzia tetesi kuzungumzia tetesi katika kipindi ambacho bado nina mkataba na timu yangu unaomalizika mwaka 2020, nadhani ni mapema mno.”

“Ninachoweza kusema ni kwamba pamoja na kuibuka kwa tetesi hizo, bado sitarajii kucheza soka katika timu za nje ya England katika kipindi hiki cha kutumikia mkataba wangu wa sasa,” alisema Sterling.

Pia mwanandinga huyo amekataa ofa ya klabu yake hiyo waliyopanga kumlipa mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki.

Sterling ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Liverpool mwenye umri wa miaka 22, amehusishwa na tetesi za kujiunga na Real Madrid huku kukiwa na taarifa za kutakiwa pia Arsenal, Chelsea, PSG na Juventus.

No comments