Habari

RIVALDO USO KWA USO NA MESSI, NEYMAR NA SUAREZ NDANI YA BARCELONA

on

Ulikuwa ni ‘mkutaniko’ wa nyota mashuhuri wa zamani na wa sasa ndani uwanja wa mazoezi ya Barcelona Jumatano asusbuhi.
‘Lejendari’ wa Kibrazil mshambuliaji   Rivaldo, ambaye alikuwa na miaka mitano isiyosahaulika ndani ya  Nou Camp kati ya mwaka 1997 na 2002, alitinga kwenye mazoezi ya Barcelona wakati mabingwa hao wa Hispania walipokuwa wanajiandaa kwa mchezo wa robo fainali ya ‘Spanish Cup’ dhidi  Real Sociedad utakaopigwa Alhamisi usiku.
Mkali huyo mwenye umri wa miaka 44 akawatia wazimu mashabiki wa Barcelona pale alipotuma mtandaoni iliyomuonyesha akiwa Lionel Messi, Neymar and Luis Suarez, na kisha akaongeza herufi ya jina lake kwenye ile MSN – herufi tatu zinazotambulisha safu kali ya washambuliaji hao watatu wa Barcelona (Messi, Suarez na Neymar).
Rivaldo akaisindikiza picha hiyo na maandishi yaliyosema:  “Asanteni kwa mapokezi yenu na upendo ambao wachezaji wote mliuonyesha kwangu …Visca Barca! MRNS”. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *