"RIYAD MAHREZ NA WENZIO MMELEWA SIFA, MNAZINGUA HAMNA LOLOTE!"

BAADHI ya wadau wa soka wanadhani kuwa wachezaji wa timu ya Algeria inayoongozwa na mchezaji bora wa Afrika, Riyad Mahrez na mastaa wengine kibao, wamelewa sifa na kudhani wao ndio wao ndio maana wameshindwa kufanya vyema kwenye michuano ya mwaka huu ya Afrika.

Algeria waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kufuzu fainali za mwaka huu za Afrika kutoka Kundi B wakipiga pia chapuo la ubingwa, wana hatihati ya kufika hata robo fainali.


Walianza kwa sare ya 2-2 na Zimbabwe kabla ya kuchapwa na Tunisia 2-1 na sasa watakamilisha hatua ya makundi kwa kumenyana na Senegal ambayo imeshafuzu baada ya kushinda mechi zote mbili za awali.

No comments