RIYAMA ALLY ATAMBA HAWEZI KUCHUJA KWENYE BONGOMUVI

MWIGIZAJI machachari wa filamu Bongo, Riyama Ally hawezi kuchuja kwenye Bongomuvi kutokana na kile alichodai kwamba anajua na anazingatia miiko ya sanaa.

Amesema kuwa ana mambo mengi yanakuja na amejipanga kupaa zaidi katika fani hiyo kwa mwaka huu 2017.

“Mimi ninajua miiko ya sanaa, jambo ambalo linanifanya nizidi kung’ara kwenye filamu na pia uigizaji ni kazi yangu ya maisha na siifanyi kwa mzaha,” alisema Riyama.


Mwigizaji huyo alisema kuwa, kwa kuzingatia miiko yote ya sanaa hatarajii kuchuja haraka kama ambavyo baadhi ya wasanii wamekuwa wakipotea ghafla kwenye sanaa kwa kutozingatia miiko.

No comments