RONALDO ASIKITIKA LIONEL MESSI KUKOSA KUHUDHURIA SHEREHE ZA MWANASOKA BORA LAKINI "AMEMSAMEHE"

MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amesema amewasamehe  Barcelona kwa kushindwa kuhudhuria sherehe za Mwanasoka Bora wa Dunia wa Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA).

Nahodha wa Barcelona, Andreas Iniesta alituma salamu za kuomba radhi kwa kukosekana kwa nyota wa timu hiyo na kujitetea kuwa walikuwa wanakabiliwa na mechi muhimu ya Kombe la Copa Del Rey.

Hata hivyo, wachunguzi wa mambo wanachukulia sababu kubwa ni hasira ya nyota hao kwa kitendo cha Lionel Messi kukosa tuzo hiyo ambayo ilinyakuliwa na Ronaldo anayechezea mahasimu wao, Real Madrid.


“Nimesikitika nyota wa Barcelona kutokuwepo hapa kwani ningependa sana Messi awepo hapa. Ila nimewaelewa kwani wana mechi muhimu,” alisema Ronaldo ambaye kauli yake hiyo ilitafsiriwa kama kijembe kwa Barcelona.

No comments