Habari

RONALDO MCHEZAJI BORA WA FIFA, CLAUDIO RANIERI KOCHA BORA …La Liga bado yaikimbiza dunia

on

Supastaa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mwanasoka bora wa FIFA na kuwabwaga Lionel Messi wa Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid.

FIFA THE BEST 2016 AWARD WINNERS 

Men’s Player – Cristiano Ronaldo
Women’s Player – Carli Lloyd
Men’s Coach – Claudio Ranieri
Women’s Coach – Silvia Neid
Fair Play award – Atletico Nacional
Award for Outstanding Career – Falcao
Puskas Award – Mohz Faiz Subri
Fab Award – Borussia Dortmund and Liverpool supporters
FIFAPro World11 – Manuel Neuer, Dani Alves, Marcelo, Gerard Pique, Sergio Ramos, Andres Iniesta, Toni Kroos, Luka Modric, Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Luis Suarez  

Kocha wa Leicester City Claudio Ranieri naye ameibuka kidedea kwa kuchaguliwa kuwa kocha bora wa FIFA.

Kikosi cha wachezaji bora 11 wa FIFA nacho kimetajwa ambapo kwa mara nyingine wachezaji wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga) wamesheheni katika orodha hiyo.

Nyota wanaounda kikosi cha FIFA ni  Manuel Neuer, Dani Alves, Marcelo, Gerard Pique, Sergio Ramos, Andres Iniesta, Toni Kroos, Luka Modric, Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Luis Suarez.

Ukiondoa kipa Manuel Neuer wa Bayern Munich na beki Dani Alves wa Juventus, wengine wote waliosalia wanatokea La Liga.

Ligi yenye mashabiki wengi duniani – Premier League ya England, haijatoa hata mchezaji mmoja.

Mtoto wa Ronaldo – Cristiano Ronaldo Jnr akishika tuzo ya baba yake kwa shauku huku dada wa Ronaldo Elma akishuhudia

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *