ROSE NDAUKA AJIANDAA KUACHIA MUVI MPYA YA FUNGUA MWAKA

BAADA ya kimya cha zaidi ya nusu mwaka, mwigizaji nyota wa Bongomuvi, Rose Ndauka anajiandaa kuipua filamu mpya ambayo itakuwa ni ya kwanza mwaka huu wa 2017.

“Filamu yangu ya mwisho ilikuwa inaitwa “Angela” ambayo niliitoa Mei, mwaka jana na tangu hapo nimekuwa kimya na sasa ninakuja na nyingine ambayo bado sijaipa jina,” alisema Ndauka.

Alisema, kimya chake kilitokana na kuzidiwa na majukumu na anarudi kwa kasi kwa vile anaamini kuwa Bongomuvi bado inalipa ingawa baadhi ya wasanii wamekuwa wakidai kuwa imekufa.


“Bongomuvi bado inalipa, cha msingi ni msanii kuandaa kazi zenye ubora. Mimi ninajiandaa kushuti filamu yangu mpya inaweza kuwa ndio pekee kwa mwaka 2017 au nitaongeza ya pili kama itawezekana,” alisema.

No comments