SAIDA KAROLI ATOA RUKSA WASANII “KUIBA” NYIMBO ZAKE… adai ni heshima kubwa kwake

NYOTA wa muziki wa asili ya kabila la Kihaya, Saida Karoli amesema kuwa hana mpango wa kuchukua hatua zozote za kisheria dhidi ya wasanii wanaotumia vionjo na mashairi kutoka katika nyimbo zake zilizowahi kutamba.

“Wanaofanya hivyo waendelee tu kwasababu ni jambo jema kwani wanaonyesha heshima katika muziki wetu katika kuufikisha kwenye levo za kimataifa,” alisema Saida.

Alisema kuwa hana wivu na mambo ya ubunifu katika sanaa na ndio maana anajisikia raha kuona Diamond Platnumz amerudia wimbo wa “Maria Salome” ambao yeye (Saida) alitamba nao miaka iliyopita.

Saida alisema kuwa wimbo huo kwa sasa haumtangazi Diamond bali hata yeye (Saida) aliyeutunga, kwa vile anaamini kwamba Diamond anapoulizwa kuhusu wimbo huo asili yake itabidi amtaje mtunzi wake.


Alisema, anafahamu kuwa wimbo wa “Muziki” wa msanii darasa una vionjo vya “Maria Salome” kama ulivyo pia wimbo “Give It To Me” wa Belle 9 na akasisitiza kwamba wasanii wanaotamani kutumia vionjo vya nyimbo zake wasisite kuvitumia.

No comments