SANAMU LA LIONEL MESSI ARGENTINA LAVUNJWA NA VIBAKA

SANAMU la staa Lionel Messi iliyojengwa nchini Argentina imevunjwa na vibaka.

Sehemu ya juu ya sanamu hiyo ya nyota huyo wa Barcelona imevunjwa na vibaka hao ambao wamebakiza sehemu ya miguu na mpira.

Vibaka hao wamevunja sehemu za kichwa, mwili na mikono na kuondoka navyo.


Sanamu hiyo ya Messi ilijengwa Juni, 2016 baada ya kutangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa ya Argentina.

No comments