SANCHEZ NAE ANUKIA JELA KUTOKANA NA TUHUMA ZA UKWEPAJI KODI

KESI za wachezaji, hasa wa Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga kukwepa kodi ni jambo la kawaida.

Na hii inaonekana hasa kwa wachezaji wa Barcelona. Lionel Messi na Mascherano ni kati ya wachezaji ambao siku za hivi karibuni wamekumbana na kesi za namna hii.

Messi alikumbwa na kashfa kubwa ya kukwepa kodi akienda mahakamani mara kadhaa. Hii ilikuwa kero kubwa kwa Lionel kwani ilifikia hatua akaanza kuiona Ligi ya Hispania kuwa chungu na kuhusishwa kuhama.

Alexis Sanchez nae ameingia kwenye mlolongo huo kupitia video. Sanchez amekiri mahakamani Hispania kwamba alikwepa kiasi cha pauni 900,000 alipokuwa akiitumikia Barcelona.

Sanchez amekiri kufanya kosa hilo akiwa Barca kabla ya kuja Uingereza kujiunga na Arsenal.

Ukwepaji kodi unaonekana ni kasumba kwa wachezaji wanaotoka bara la amerika ya Kusini na pengine hii inachangiwa na aina ya maisha waliyopitia utotoni.

Inasemekana Sanchez mwenye miaka 28, alificha uhusiano wake na kampuni ya Numidia mwaka 2012, kuficha uhusiano huko na Numidia kulimsaidia kukwepa kulipa pauni 516,190 na kukwepa tena pauni 347,642 mwaka 2013 japokuwa baadae alilipa kiasi chote hicho.

Sasa Sanchez atatakiwa kulipa faini kubwa ili kutopata kesi kubwa. Mawakili wake wanatarajiwa kukutana na mahakama Hispania kukubaliana kiasi cha faini ambayop inaonekana itakuwa kubwa kwa kuwa alichelewa kukitri kosa hilo.


Sasa Sanchez atahukumiwa kwenda jela japokuwa kwa sheria za Hispania hukumu ya kifungo cha chini ya miaka miwili unatumikia ukiwa mtaani.

No comments