SANTI CAZORLA “AIUMIZA” ARSENAL... haijulikani pengo lake litazibwa vipi

WAKATI Arsenal ikiwa na nafasi ngumu ya kutwaa ubingwa wa England, hivi sasa kuna swali linaulizwa kuwa timu hiyo itaziba vipi pengo la kiungo wake Santi Cazorla.

Cazorla alifanyiwa operesheni ya enka ya mguu wa kulia Desemba 7, mwaka jana nchini Sweden na atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Kufuatia pengo lake timu hiyo imekuwa inasuasua na hivi karibuni ilipoteza mechi mbili dhidi ya Everton na Manchester City na kuifanya kupoteza mwelekeo wa kutwaa ubingwa.

Cazorla anaweza kuwa sio mchezaji bora lakini ni muhimu katika kikosi hicho na hasa linapokuja suala la uchezeshaji wa timu.


Kiungo huyo anategemewa sana na Arsenal na hasa katika kumiliki mpira na kuongoza mashambulizi ambapo kukosekana kwake kumeiathiri timu kwa kiasi kikubwa.

No comments