SENEGAL, CAMEROON KUVAANA ROBO FAINALI KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

SENEGAL itavaana na Cameroon katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakayopigwa Jumamosi.

Timu nyingine zilizofuzu kwenye robo fainali ni Tunisia na Burkina Faso ambazo pia zitavaana Jumamosi.

Senegal ilifikia hatua hiyo baada ya kuongoza Kundi B kutokana na kuwa na pointi saba baada ya kufungana mabao 2-2 na Algeria juzi.

Mechi hiyo inatazamiwa kuwa na mvuto kutokana na kuikutanisha miamba hiyo ya soka barani Afrika iliyokabiliana kwenye fainali ya mwaka 2002 ya michuano hiyo.

Tunisia iliyokamata nafasi ya pili katika Kundi B licha ya kuicharaza Zimbabwe mabao 4-2, inakabiliana na Burkina Faso walioongoza Kundi A wakifuatiwa na Cameroon.


Algeria ni miongoni mwa timu zilizokuwa zinapewa nafasi kubwa kutwaa taji hiyo, iliaga mashindano hayo kutokana na kuambulia pointi mbili tu, kiasi cha kocha wake, George Leekens kuamua kuachia ngazi.

No comments