SERENA WILLIAMS SASA AMECHOKA, AAMUA KUMWANIKA MCHUCHU WAKE

HATIMAYE baada ya fununu za muda mrefu, nyota tenisi duniani, Serena Williams ameweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi na mmoja wa waanzilishi wake, Alex Ohanian kwenye mtandao wa kijamii.

Katika shairi aliloliweka katika ukurasa wake, aliandika namna alex alivyompeleka katika mgahawa mmoja mjini Rome, eneo ambalo walikutana kwa mara ya kwanza mwaka mmoja uliopita.

Siku ambayo alipiga magoti na kuweka pete kwenye kidole chake na kusema maneno manne na yeye akasema “ndio”, yametimia.

Mwezi Julai mwaka huu, Serena alishinda medali ya Wimbledon kwa mara ya saba na mwezi wa Sptemba aliweza kuchukua nafasi ya Rogel federer’ ambaye alikuwa mshindi wa mechi za Grand Match kwa kipindi kirefu.

Awali kulikuwa na fununu kwamba mwanamichezo huyo hakuwa katika nia yoyote ya kuolewa kwasababu amezoea maisha ya kujirusha akiwa na wanaume tofauti, madai ambayo yamekuwa yakipingwa na Serena kila mara.

No comments