SERGIO AGUERO AWAGONGANISHA BINTI WA MARADONNA NA DEMU WAKE WA SASA

KUFUATIA kufungiwa mechi nne na kichapo cha siku ya mwaka mpya dhidi ya Liverpool, mtihani mpya alionao straika wa Manchester City, Sergio Aguero ni kutuliza bifu lililoibuka baina ya mkewe wa zamani, Gianinna Maradonna, binti wa Diego na demu wake wa sasa, Karina, mwimbaji wa Kiargentina.

Wawili hao wametumia kurasa zao za Twitter kumwagiana povu kufuatia binti wa Karina aitwae Sol kugombana na Benjamin, mtoto ambaye Aguero alizaa na mkewe huyo wa zamani.

“Kama una jambo unataka kusema kuhusu binti yangu nipigie simu uniambie,” Karina aliandika ujumbe wa Twitter kwa Gianinna Maradonna.

“Mimi nayamudu hayo, ruksa kulichafua jina langu utakavyo lakini usimuhusishe binti yangu.”

Gianinna Maadonna awali alisisitiza kwamba asingejibizana kupitia Twitter lakini siku moja baadae akawa na cha kusema.

“Watoto huiga tabia za wazazi wao na yeye aliyebahatika kumfahamu Benjamin atakwambia mimi ni mtu wa aina gani kama mama,” alisema.

“Benjamin ni mtu poa sana, mtulivu na pia ni rafiki mzuri, mtoto na mjukuu mwema.”

Mchezaji huyo hajajibu bifu hilo la kwenye mtandao wa kijamii.

No comments