SERGIO RAMOS NA IMANI KIBAO ZA NGUVU ZA GIZA

WANASOKA mara nyingi huwa na imani za giza na Sergio Ramos ni mmojawao.

Beki huyo wa Real Madrid amebainisha kuwa hutanguliza mguu wa kushoto kuingia kwenye dimba la uwanja kabla ya mechi na pia huwapigia simu awapendao kabla hajaingia uwanjani kuitumikia klabu yake au timu ya taifa ya Hispania.

“Kabla ya kila mechi ninawapigia simu familia yangu, mke na wanangu, baba yangu. Na baadae nasikiliza muziki kidogo. Nikielekea kuingia dimbani daima natanguliza mguu wangu wa kushoto.”

Wakati imani ya Ramos ikiwa hivyo, nyota wa Manchester United, Ander Herreera, 27, amejikuta akigeuzwa kituko cha wachezaji wenzake ambao humcheka kutokana na kuvaa vikinga ugoko (shin pads) hizohizo anazovaa tangu akiwa na umri wa miaka minane.


“Nitaendelea kuvaa hizi hadi zitakaposambaratika kabisa,” alisema.

No comments