SHAMSA FORD ASEMA MATABAKA NDANI YA BONGOMUVI YANACHANGIA KUWAKWAMISHA WASANII KIMAENDELEO

MWIGIZAJI wa filamu, Shamsa Ford anasema kuwa matabaka yaliyoko ndani ya Bongomuvi yanachangia kukwamisha maendeleo ya tasnia hiyo kwa wasanii.

Amesema kuwa umefika wakati sasa wasanii wa filamu waache matabaka na kujiona kama kitu kimoja ili kusaidiana katika kazi na kuhakikisha Bongomuvi inarudi kwenye chati.

“Wapo baadhi ya wasanii wanaojiona kuwa wao ni bora kuliko wengine na ni wagumu kuwapa wenzao namba zao za simu wakati wako kwenye tasnia moja, hali ambayo naiona inachangia kukwamisha ushirikiano,” alisema Shamsa.


Alisema, wito wake kwa wasanii wenzake ni kwamba wanapouanza mwaka huu mpya wa 2017 wabadilike, waache matabaka na kuungana kwa ajili ya kuendeleza fani yao ambayo ina mashabiki wengi hadi nje ya nchi.

No comments