SHIKAMOO JAZZ YA SALUM ZAHOR KUUNGURUMA EUROPE BAR BUGURUNI LEO

SHIKAMOO Jazz inayotumia mtindo wa “Chelachela Beat” jioni hii inatarajiwa kuwasha moto mkali wa burudanio ndani ya ukumbi wa Europe Bar, Buguruni Sokoni, jijini Dar es Salaam.

Bendi hiyo inayokusanya wakongwe wengi wa muziki, wakiwemo Salum Zahor, Ally Adinani na Suleiman Majengo, itaangusha burudani hiyo kuanzia majira ya saa 1:00 na kuendelea hadi saa 6:00 usiku.

Taarifa kutoka ndani ya bendi hiyo zinasema kuwa, shoo hiyo ni maalum kwa ajili ya mashabiki wao wa kitongoji hicho cha Buguruni na Wilaya nzima ya Ilala kwa ujumla.

Pamoja na kufaidi vibao vyetu mbalimbali, lakini pia watakaohudhuria watapata nyimbo mbalimbali za zamani zilizopigwa na bendi nyingine ndani na nje ya Afrika,” amesema taarifa hiyo.

No comments