SHILOLE: ACHENI KULIA NA UGUMU WA MAISHA, JITUMENI VIJANA WENZANGU

MWIMBAJI wa muziki wa Kizazi Kipya, Zuwena Mohammed “Shilole” amewataka vijana waache kulalamika kuwa maisha ni magumu na badala yake wajitume kwa kufanya shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato.

Katika ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo ameeleza kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wakilalamika kuwa pesa hazipatikani huku wakiwa wamebaki kukaa vijiweni pasipo kuhangaika kutafuta njia za kuwaingizia kipato.

“Mtu unalalamika hali ngumu huku umekaa kijiweni bila kujishughulisha, hivi kweli pesa zinaweza kupatikana kwa njia hiyo?” alihoji msanii huyo anayetamba na wimbo “Mtoto Mdogo”.


Alisema kuwa yeye hachagui kazi ilimradi iwe halali na ana aibu na sasa ameanza kuonja matunda ya kujituma kwake kwenye kazi hadi amefikia kuwa na uwezo wa kujenga nyumba.

No comments