SIKINDE NGOMA YA UKAE KUINGIA MAFICHONI KESHO KUPIKA NYIMBO MPYA

SIKINDE Ngoma ya Ukae kesho Jumatano wanatarajiwa kuanza mazoezi ya nyimbo zao mpya kabisa, ikiwa ni katika harakati za kujiandaa na albamu yao mpya, imefahamika.

Kiongozi mwandamizi wa Sikinde, Abdallah Hemba ameieleza Saluti5 kuwa tayari wana nyimbo kadhaa mpya kutoka kwa baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo ambapo kesho wataamua ya kuanza nayo.

“Mimi binafsi nina wimbo wangu unaozungumzia maisha kwa ujumla wake, kwahiyo kesho tutaangalia tuanze na wimbo wa nani, lakini lengo ni kwamba tuwe na vibao sita hadi vinane katika albamu ijayo tutakayoiachia Juni, mwaka huu,” amesema Hemba.


Hadi sasa Sikinde ambao ni hasimu wa Msondo Ngoma Music Band wana vibao viwili ambavyo ni “Wali Nazi” (Karama Regessu) na “Naisubiri Bahati” (Habib Abbas Jeff), vinavyoonekana kuchengua vilivyo mashabiki wao kwenye kumbi mbalimbali wanazotumbuiza.

No comments