SIKINDE NGOMA YA UKAE NDANI YA SAFARI RESORT KIMARA LEO

WAKONGWE wanaotikisa anga la muziki wa dansi nchini, Mlimani Park ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’ leo wanatazamiwa kuwasha moto mkubwa wa burudani ndani ya Safari Resort, imefahamika.

Safari Resort ni ukumbi maarufu wa burudani ulioko Kimara Korogwe jijini Dar es Salaam, ambao ulizindua upya shughuli za burudani jana Jumamosi kwa dansi la kufa mtu kutoka kwa FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

Taarifa kutoka ndani ya ukumbi huo zinasema Sikinde waliojipanga kutoa burudani kali, watawaonyesha mashabiki wao wa Kimara kile ambacho walikikosa tangu mwaka 1996 wakati ukumbi huo uliposiomamisha rasmi shughuli za burudani na kubakia na huduma ya vinjwaji na chakula tu (Bar).


Taarifa hiyo imewaomba mashabiki, wapenzi pamoja na wadau wote kufika kwa wingi leo ili kujifaidia uhondo wa burudani pevu ambao wana Sikinde Ngoma ya Ukae umeuandaa kwa ajili yao.

No comments