SIMBA YAING’OA YANGA MAPINDUZI CUP …matuta bado ni donda ndugu Jangwani


Simba imeng’oa Yanga katika michuano ya Mapinduzi Cup katika mchezo wa nusu fainali uliolazimika kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti (4-2) baada ya kutoka sare ya 0-0  ndani ya dakika 90 za kawaida.

Katika mchezo huo uliochezwa Amani Stadium, Zanzibar, timu zote zilijizatiti kwenye ulinzi huku mashambulizi yakiwa adimu kwa kila upande.

Yanga ambayo imekuwa ikichukua kipigo katika mechi nyingi zinazoamuliwa kwa 'matuta', itabidi ijilaumu yenyewe katika upangaji wa wapigaji wa penati.

Benchi la ufundi la Yanga liliwaacha nyums Haruna Niyonzima, Amis Tambwe na Kelvin Yondan  ambao wanarekodi nzuri ya mikwaju ya penalti na kuwatanguliza Deogratius Mushi “Dida” na Mwinyi Hajji ambao uwezo wao wa mashuti ya penalti unatia shaka.

Jonas Mkude, kipa Daniel Agyei, Muzamil Yassin na Janvier Besala Bokungu ndio waliodumbukiza wavuni penalti za Simba huku penalti ya Method Mwanjali ikiokolewa na kipa wa Yanga, Deogratius Munishi “Dida”.

Kipa wa Simba  Daniel Agyei aliyesajiliwa kutoka Ghana,  ndiye aliyekuwa shujaa kwa kupangua penalti  za Dida na Mwinyi Hajji wakati Simon Msuva na Thabani Kamusoko ndio waliofunga penalti za Yanga.

Simba sasa itaumana na Azam katika mchezo wa fainali utakapigwa siku ya Ijumaa katika dimba hilo hilo la Amani.

Simba: ⁠⁠Daniel Agyei, Janvier Bokungu, Mohammed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Shiza Kichuya (Jamal Mnyate), James Kotei, Juma Luizio (Pastory Athanas), Muzamil Yassin na Mohamed Ibrahim (Laudit Mavugo).


Yanga: Deogratius Munishi, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Andrew Vincent, Kelvin Yondan, Saidi Juma Makapu, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe, Haruna Niyonzima na Deusi Kaseke (Emmanuel Martin).

No comments