SIMBA YAKATAA KUIKWEPA YANGA, YAIFUATA NUSU FAINALI …Mavugo ‘afufuka’ Jang’ombe ikilala 2-0


SIMBA imeifuata Yanga katika nusu fainali ya Mapinduzi Cup baada ya kuitungua Jangombe Boys 2-0 kwenye mchezo wa kundi A.

Tofauti na ilivyodhaniwa na wengi kuwa Simba ingelazimisha sare ili kuikwepa Yanga, klabu hiyo ya Msimbazi ikasaka ushindi kwa udi na uvumba na kutupia bao moja katika kila kipindi.

Katika mchezo huo uliochezwa Amani Stadium huko Zanzibar, mshambuliaji Laudit Mavugu ndiye aliyeibuka shujaa kwa kufunga magoli yote mawili.

Nusu fainali zitachezwa Jumanne ambapo mechi ya Simba na Yanga itapigwa saa 2 na robo usiku.

No comments