SNURA ATAMANI KOLABO NA SHILOLE... asema bifu lililokuwa kati yao lilishamalizika siku nyingi

NYOTA wa filamu na muziki wakizazi kipya Snura amesema anatamani kufanya kazi na Shilole kwa vile bifu lililokuwa kati yao lilishamalizika siku nyingi.

Snura alisema hayo wakati akiojiwa na kituo kimoja cha redio na fufafanua kuwa bifu lao yalikuwa mambo ya zamani sana na walishayamaliza na sasa wako sawa na hawawezi kugombana na pia muziki wao haufanani.

“Natamani sana kufanya kazi na Shilole ikiwezekana tufanye wimbo wa pamoja ama filamu kwa kuwa yeye ni msanii mzuri wa kuigiza naamini tukifanya hivyo tutatengeneza pesa nzuri,” alisema Snura.


Alisema kuwa kila mara amekuwa akijitahidi kumtafuta Shishi Baby kwa lengo la kumweleza nia yake hiyo lakini bado inaonekana kimwana huyo bado hajawa tayari kushirikiana katika kazi.

No comments