SNURA AWAPA MBINU WASANII WA KIKE ZA KUWAKWEPA WANAUME WAKWARE

STAA wa filamu na muziki wa kizazi kipya, Snura Mushi amesema njia pekee itakayowasaidia wasanii wa kike kukwepa mitego ya wanaume wakware ni kuwa mbali nao.

Snura alisema kuwa ana uhakika wasanii wa kike wamekuwa wakikumbana na vishawishi vingi katika muziki kama ilivyo kwake, lakini bahati nzuri amekuwa akikabiliana navyo na kuvishinda.

“Mimi nimekuwa nikipata usumbufu kutoka kwa wanaume lakini ninadhani kwamba wengi wao hawana nia ya mapenzi ya kweli, hivyo ninajitahidi kukaa nao mbali ndio maana ninawashauri wasanii wenzangu wa kike kuzingatia hilo,” alisema Snura.


Alisema kuwa kwenye muziki kuna vishawishi vingi ambavyo msanii wa kike asipokuwa makini anaweza kujikuta akipotea kwa kujitumbukiza katika mambo mengine ambayo hayana manufaa kwake. 

No comments