SOL CAMPBELL AFUZU MAFUNZO YA UKOCHA, APANIA MAKUBWA


Sol Campbell amekamilisha mafunzo ya ukocha na kupata beji ya UEFA na sasa anasema anataka kuwa kocha (meneja) bora kuliko wote ambao England imewahi kuwatengeneza.

Sentahafu huyo wa zamani wa England, Tottenham na Arsenal, amesema ana uchu wa kurejea kwenye mchezo huo uliomfanya awe staa.

Moja ya jambo muhimu analotaka kufanya Sol Campbell mwenye umri wa miaka 42, ni kutoa ushauri nasaha kwa mchezaji chipukizi wa Manchester City John Stones  ili awe beki bora duniani.
No comments