SSERUNKUMA APANIA KUWEKA REKODI FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

STRAIKA wa timu ya taifa ya Uganda, Geoffrey Sserunkuma amepania kuweka rekodi kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Alikuwa Mganda wa kwanza kufunga kwenye fainali hizo tangu nchi hiyo ilipofuzu fainali hizo kwa mara ya mwisho mwaka 1978.

Uganda imepangwa katika Kundi gumu la D ikiwa na timu za Ghana, Misri na Mali.

Sserunkuma anayechezea KCCIA ndie anayeongoza kwa kufunga mabao kwenye Ligi Kuu Uganda akiwa na magoli nane.

“Nimepania kufunga AFCON (Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika), ili niweke rekodi ya Uganda,” alisema Sserunkuma.

No comments