STEVE NYERERE ASEMA 2017 KUANZA TENA KUTOA MUVI MOJA KILA MWAKA

STEVE Nyerere amekiri kushindwa kutimiza ahadi yake ya kutoa filamu moja kila mwaka na sasa amesema kuwa anajipanga kuhakikisha hachemki tena mwaka 2017.

Mwanzoni mwa mwaka jana msanii huyo aliahidi kutoa filamu moja lakini ahadi hiyo haikutimia kutokana na kile alichodai kuwa ni sababu ambazo ziko juu ya uwezo wake.

“Ahadi yangu ya kutoa filamu moja kwa mwaka itatimia mwaka huu kwa sababu sikufanya hivyo mwaka jana kutokana na mambo yaliyoingilia kati na kunilazimisha kuhairisha kimyakimya,” alisema.

Mchekeshaji huyo alisema kuwa msimamo wake wa kutoa filamu moja kwa mwaka unalenga kuhakikisha anatoa kazi yenye ubora wa hali ya juu na inayokubalika kwa mashabiki wa tasnia hiyo.


“Kutoa filamu kila baada ya mwezi ama baada ya miezi mitatu ni sawa na kulipua na nimekuwa nikiwashauri wenzangu kuachana na mtindo huo na kujipa muda wa kutosha wa kuandaa kazi nzuri,” alisema.

No comments