TORRES ASEMA UAMUZI WA KUREJEA ATLETICO MADRID NI MPANGO WA MAANA KWAKE

FERNANDO Torres amesema uamuzi wake wa kurejea katika klabu yake ya zamani ya Atletio Madrid ni mpango wa maana na anajisikia faraja kuona mambo yanaendelea kumnyookea.

Kisha akakiri kupanda kwa kiweango chake kiasi cha kurudisha makali yake ya kupachika mabao hata kuisaidia timu yake hiyo.

SKY Sport wameripoti kuwa Fernando Torres anajisikia furaha kuwa Madrid kuliko alivyokuwa katika klabu nyingine zote alizowahi kuzitumikia ikiweme Chelsea.

Torres alikuwa akikipiga kwa mkopo katika klabu ya AC Millan akiwa mali ya The Blue ya England kabla ya kuhama kurejea katika LaLiga.

Hakuonyesha mafanikio ambapo tangu atue ana bao moja tu katika michezo kumi na alipata nafasi ya kupangwa katika kikosi cha kwanza.


“Ni kama nimezaliwa upya, nikiwa hapa Atletiko Madrid ni wakati wangu wa kuangalia maisha mapya ya kikosi na hasa nikiamini nimerudi katika klabu iliyonipa jina na mafanikio makubwa,” alisema Torres.

No comments