TUNDAMAN AANZA KUSHUTI VIDEO YAKE YA "MWANAUME SURUALI"

TUNDAMAN ameanza kushuti video ya wimbo wake “Mwanaume Suruali” ambayo alilazimika kuisimamisha kwa muda baada ya Mwana FA kutoa wimbo wake unaotamba sasa wa “Dume Suruali”.

Msanii huyo alisema kuwa alianza kutangaza ujio wa “Mwanaume Suruali” mapema mwaka 2016 na ndio ulitakiwa kutoka kabla ya mwingine wa “Debe Tupu” ambao tayari uko sokoni.

“Lakini kabla ya “Mwanaume Suruali” haujatoka alikuja mwelekezaji wa video na kunambia Mwana FA ana wimbo ambao una ujumbe unaofanana na wangu, akaniomba nimpe nafasi na tayari ameshatoa video, hivyo sasa ni zamu yangu ya kuendelea na huu wa kwangu,” alisema Tundaman.

Aliongeza kuwa amelazimika kuufanyia mabadiliko kidogo wimbo wake huo ili utofautiane na ule wa Mwana FA kwa madai kuwa aliusikiliza “Dume Suruali” na kubaini baadhi ya vitu vinafanana.

No comments