TWANGA PEPETA ‘KUITEKA’ ZENJI JUMAMOSI HII …ni baada ya ‘game’ ya Yanga na Azam


The African Stars “Twanga Pepeta” Jumamosi hii watavuka maji na kwenda  kukinukisha Zenji ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.

Twanga Pepeta watatumbuiza katika ukumbi wa Gymkhana ambapo nyimbo mpya kabisa za bendi hiyo zitatambulishwa.

Uhondo huo wa Twanga utarindima muda mfupi baada ya mechi ya soka ya Yanga na Azam itakayochezwa visiwani humo katika Uwanja wa Amani.

Kwa mujibu wa ripota wa Saluti5 kutoka Zenji, Show hiyo Twanga imekuwa gumzo na inasubiriwa kwa hamu kubwa.

Mashabiki wengi wa soka kutoka Dar es Salaam ambao wamekwenda Zenji kwaajili ya mechi ya Yanga na Azam itakayochezwa saa 2.30 usiku, nao wamefurahishwa na uwepo wa onyesho hilo la Twanga, huku wengi wao wakitarajiwa kujitosa Gymkhana Club mara baada mtanange wa Amani Stadium kukamilika.

No comments