Bendi ya The African Stars “Twanga Pepeta” imerejesha bonanza lake lake la kija Jumapili ambapo sasa litakuwa linapatikana ndani ya Mzalendo Pub, Millennium Tower, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Twanga itakuwa inarindima katika ukumbi huo wa magorofani uliokarabatiwa upya kila Jumapili kuanzia saa 12 jioni hadi usiku mnene.

Jumapili hii itakuwa ni wiki ya nne mfululizo kwa Twanga Pepeta kupiga hapo na tayari onyesho hilo limeanza kuwa gumzo la jiji.

Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka ameiambia Saluti5 kuwa Mzelendo Pub ni sehemu bora zaidi ya kujiachia kila Jumapili kutokana na mandhari ya ukumbi, usalama pamoja na ‘parking’ ya kutosha kwa wanaokwenda na vyombo vyao vya usafiri.

Ukiachana na onyesho hilo la Jumapili, ule uhondo wa Twanga Pepeta kila Jumamosi ndani ya Mango Garden Kindondoni uko pale pale ambapo wajanja wote wa mjini hukutana hapo.


USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac