UNAJUA KWANINI CONTE ALIMWEKA PEMBENI DIEGO COSTA MECHI YAO DHIDI YA LEICESTER CITY?

WIKIENDI hii mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Chelsea, Diego Costa aliachwa na kocha Conte kwenye mechi dhidi ya Leicester City kutokana na kutokuwa na maelewano.

Inasemekana kwamba Costa aligomea mazoezi ya viungo ya kocha huyo na kutupiana maneno ambapo mwisho wa siku kocha aliamua kumuacha katika kikosi hicho.

Sababu nyingine inasemekana Costa anataka kwenda China ambako ameahidiwa mshahara mkubwa na hivyo ameanza kumdengulia mwalimu wake.


Kutokana na taarifa mpya kwenye kikosi hicho ni kwamba wachezaji wa Chelsea wamemjia juu mchezaji huyo na kumtaka amalizane na kocha wao.

No comments