UPACHIKAJI MABAO WAMPA "UJIKO" MSHAMBULIAJI JUNIOR KABANANGA WA KONGO (DRC)

MSHAMBULIAJI wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC), Junior Kabananga amegeuka kuwa lulu ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Kabananga ambaye kabla ya mashindano hayo alikuwa hatajwi amejizolea sifa kutokana na kuongoza kwa ufungaji kwenye fainali hizo akiwa na mabao matatu.

Nyota huyo amefunga katika kila mechi ya mashindano hayo na kuchangia Kongo kuongoza Kundi D.

Kuna uwezekano mkubwa kwa Kabananga kupata dili kwenye timu kubwa za Ulaya ambapo kwa sasa anachezea Astana ya Kazakhstan.


Kabananga anaiongoza Kong oleo kukabiliana na Ghana kwenye mechi ya robo fainali ya mashindano hayo.

No comments