Habari

VAN GAAL ABADILISHA GIA ANGANI NA KUSEMA HAJATANGAZA KUJIUZULU UKOCHA

on

KOCHA wa zamani wa Manchester United Louis van Gaal amesisitiza kuwa hajaachana na soka bali yupo kwenye mapumziko ya mwaka mzima na atatoa hatmaya yake ifikapo Julai mwaka huu.
Van Gaal mwenye umri wa miaka 65, alikunuliwa na chombo cha habari cha Holland mapema wiki hii akisema amedhamiria kuachana na soka kwa sababu za kifamilia.
“Nafikira kuchana na soka, sitarajii kama nitarejea kwenye ukocha, alisema kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Ajax katika maongezi yake na gazeti la De Telegraaf
Lakini Jumanne usiku, Van Gaal akaenda kwenye kituo cha radio cha Cadena Ser cha Hispania na kurekebisha kauli yake.
“Hapana, hapana kabisa. Sijastaafu, nipo kwenye mapumziko ya mwaka mzima na baada ya hapo nitaamua. Itategemea na ofa nitakazozipokea. Nitatoa umaumzi mwezi Julai”,  alisema Van Gaal.
“Naweza nikarejea Hispania. Valencia walinipa ofa mwezi mmoja uliopita lakini nikasema Hapana.”
Inaeleweka pia kuwa Van Gaal alikataa ofa kwenda kufundisha China kwa dau la pauni milioni 44 kwa misimu mitatu.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *