VICENTE DEL BOSQUE AWASHUKIA WANAOMZODOA ZINEDINE ZIDANE

KOCHA wa zamani wa Real Madrid, Vicente Del Bosque amewashukia wanaomzodoa Zinedine Zidane.

Kuna wadau wa soka wamekuwa wakisema Zidane tangu ameanza kuinoa timu hiyo amekuwa anabahatisha.

Zidane amekuwa na mchango katika timu hiyo katika kuisaidia kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya “Europe Super Cup” na Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia.

“Nashangaa watu wanaosema kuwa Zidane anabahatisha wakati timu imecheza bila ya kupoteza mechi nyingi chini yake na ameleta mataji makubwa,” alisema Del Bosque.


Bosque alikumbushia nae jinsi alivyokuwa anadharauliwa wakati alivyokuwa anainoa Real Madrid na kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Hispania mara mbili, taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili, Europe Super Cup na Klabu Bingwa ya Dunia.

No comments