WAIMBAJI NI TATIZO SUGU SHOW ZA TWANGA PEPETA MIKOANI …yaenda na waimbaji watatu Zenji


ONYESHO la Twanga Pepeta huko Zanzibar jana usiku, linatajwa kuwa moja ya show za bendi hiyo iliyopwaya sana kutokana na uchache wa waimbaji.

Twanga Pepeta ilikwenda na waimbaji watatu tu – Hajj Ramadhan, Kalala Jr na Khalid Chokoraa.

Katika onyesho hilo lililofanyika katika ukumbi Gymkana, Twanga iliwakosa waimbaji wanaochukuliwa kama nembo ya bendi – Ally Chocky na Luizer Mbutu.

Hata mwimbaji wao wa ‘mkopo’ J4 Sukari pia alikosekana katika onyesho hilo.
Baada ya kuwaondoa kundini Rogart Hegga na Ferguson, Twanga Pepeta imebakiwa na waimbaji watano tu.

Tatizo la kukosekana kwa waimbaji wa Twanga katika maonyesho ya mikoani limekuwa sugu.

Katika ziara yao ya X-Mas mkoani Ruvuma, Twanga ilisafiri na waimbaji watatu tu – Ally Chocky, Luizer na Hajj Ramadhan – achilia mbali Chaz Baba aliyekwenda kama msanii mwalikwa.

Waimbaji Rogart Hegga, Ferguson (ambaye pia ni rapa), Kalala Jr na Khalid Chokoraa wote walibakia Dar es Salaam kwenye maonyesho hayo ya sikukuu ya X-Mas.

Ripota wa Saluti5 huko Zanzibar, amesema mashabiki wengi  waliohudhuria onyesho la jana, walilaani sana kukusekana kwa waimbaji mahiri Chocky na Luizer ambao ndio wanaofahamika zaidi visiwani humo.


Mshabiki mmoja ameiambia Saluti5 kuwa hata vipeperushi vilivyokuwa vikigaiwa mitaani kunadi show hiyo viliandika kuwa ni Twanga Pepeta chini ya Ally Chocky, na hivyo akashangaa kukosekana kwa mwimbaji huyo gwiji.

Wakati huo huo, habari ambazo bado hazina uthibitisho wa kutosha zinasema Chokoraa na Kalala Jr wamebaki Zenji na hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kukosekana kwenye onyesho la leo Mzelendo Pub, jijini Dar es Salaam.
 Luizer hakuwepo Zenji
Hajj BSS, Kalala Jr na Chokoraa ...waimbaji pekee wa Twanga waliokuwepo show ya Zanzibar jana 
J4 hakuwepo Zenji
Chocky hakuwepo Zenji
Kalala Jr (kushoto) na Chokoraa wamebaki Zanzibar


No comments