Habari

WAIMBAJI WA KIKE WA DANSI WANAHITAJIKA APAO RECORDS KULAMBA LEBO

on

WAIMBAJI wa kike chipukizi wa muziki wa dansi wanahitaji katika studio
za Apao Records zilizoko Mwananyamala jijini Dar es Salaam ili kulamba mkataba
ambao unaweza ukawatoa kisanii.
Mkurugenzi wa Apao Records, Richard Muro (pichani juu), ameiambia Saluti5 kuwa lengo
lake ni kuunda timu ya waimbaji watano wa dansi ambao watashiriki ‘project’
maalum ya kutengeza nyimbo za dansi la kizazi kipya.
Muro amesema kati ya waimbaji hao chipukizi, watatu watakuwa wa kiume (ambao tayari
wameshapatikana) na wawili wa kike.
“Lengo letu ni kuwapika vijana wapya wa dansi, hivyo tunahitaji waimbaji
chipukizi  na kwa bahati nzuri watatu wa
kiume wamaeshapatikana, sasa tunatafuta waimbaji wawili wa kike,” anaeleza Richard
Muro.
“Tunahitaji wawili, kwahiyo tunataka wajitokeze kwa wingi kisha
tutafanya mchujo kutokana na ubora wao,” anafafanua zaidi Muro.

Aidha, Muro ameleeza kuwa lengo la Apao si kuunda bendi bali ni
kutengeneza lebo ya waiambaji chipukizi wa dansi ili kutengeneza kazi ya mfano
ya kuonyesha ni wapi muziki wa dansi unapaswa kuelekea.
Studio za Apao ziko Mwananyamala Koma Koma jirani na ukumbi wa Kaba Kabana. Kwa maelezo zaidi piga simu No. 0714 777 727.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *