WILFRIED ZAHA ARIPOTI KAMBI YA TIMU YA TAIFA YA IVORY COAST ABU DHABI

WINGA wa Crystal Palace, Wilfried Zaha, 24, ameripoti kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ivory Coast inayojiandaa na fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Zaha ambaye amezaliwa Abidjan katika mji mkuu wa Ivory Coast, aligoma kuchezea timu ya England.

Aliwahi kuchezea England mara tatu katika mechi za kirafiki.
Zaha hata hivyo, aliamua kuachana na England baada ya kutoitwa kwa miaka mitatu.


Ameripoti kwenye kambi ya Ivory Coast ambayo iko Abu Dhabi, Falme za Kiarabu

No comments